UNAPOMTOLEA MUNGU SADAKA ZAKO NZURI UTUNZE UTAKATIFU WAKO
SOMO :
UNAPOMTOLEA MUNGU SADAKA ZAKO NZURI UTUNZE UTAKATIFU WAKO.
Bwana Yesu Asifiwe Mtu wa Mungu nichukue fursa hii kukukaribisha katika kipindi hiki cha kujifunza maneno ya MUNGU.Naamini kwa kwa kusoma ujumbe huu Mungu anaenda kubadilisha maisha yako na kukuinua zaidi KIROHO, KIELIMU,KIUCHUMI na KIUNGOZI.
UTANGULIZI
Mungu aliponena na MTUMISHI wake MUSA kuhusu kujenga maskani ya MUNGU yaani patakatifu pa patakatifu aliwaomba wana wa ISRAEL watoe sadaka/matoleo ya dhahabu,fedha/shaba/rangi mbalimbali za vitambaa,ngozi za kondoo waume n.k na wote walitoa kwa moyo wa kupenda
KUTOKA 35:1.....
- Lakini pamoja na kutoa hizo sadaka kwa MUNGU walitakiwa kutunza utakatifu wa MUNGU ndani yao kwa kutoabudu miungu mingine yoyote ile.
- Pamoja na kujitoa sana kufanya kazi ya MUNGU tunatakiwa sana kulinda UKIRISTO WETU na utakatifu wetu mbele za MUNGU , Maana kadri tunavyojitoa sana mbele za MUNGU ndivyo Mungu anavyotubariki mno na hivyo hiyo inamsababisha shetani atuchukie na kutuwinda kila saa kuangalia ni wapi tumeanguka ili atuangamize.
MIFANO
Unakuta mtu alikuwa anasoma miaka mingi kwa taabu na shida lakini baada ya kushinda mtihani wake anaamua kufanya sherehe kubwa na kuweka bajeti kubwa na kuwaarika marafiki zake kwa kula kunywa na huku wanamsahau MUNGU. Siku ya siku anakosa ajira na anaanza kumlaumu MUNGU kwamba amemuacha,kumbe alitakiwa kwanza kumpa MUNGU NAFASI YA KWANZA.
- Unakuta mtu amenunua Gari,nyumba,kiwanja,duka lakini baada ya kuvitolea sadaka kwa MUNGU anavitakasa na madhabahu za shetani kwa kutafuta waganga wa jadi kuzindika anasahau kwamba wakati anatavitafuta kabla ya kuvipata alimlilia MUNGU na MUNGU akamkumbuka na kumbariki.
Kufanya hivyo unakuwa umejifungulia mlango mkubwa kwa shetani kukushambulia nadhani umewai kuona mtu ananunua gari jipya lakini baada ya MUDA mfupi anapata ajali mbaya sana na gari linaharibika vibaya sana ushawai jiuliza kwanini???.
- Kazi ya IBILISI ni kukufuatilia ili akunyanganye kila kitu ulichobarikiwa na MUNGU hivyo anapogundua kwamba umefanya dhambi anakuharibia vyoote ulivyonavyo.
ISRAELI pamoja na kutoa matoleo mengi mno kwenye nyumba ya BWANA bado waliendelea kumwasi MUNGU akasirike na kuaangamiza woote ushawai kujiuliza kwamba kama asingekuwepo MUSA wa kuwaombea mara kwa mara ingelikuwaje si MUNGU angewawaua woote kabisa.
SOMA HI HAPA CHINI
kutoka
MUNGU alimchagua BEZALELI mwana wa URI akamjaza Roho ya MUNGU ndani yake na kumpa HEKIMA, AKILI, UJUZI na kazi ya Ustadi ya kila aina
MUNGU anaweza kukupa Akili na ukawa na Elimu Kubwa mno na Fedha za kutosha lakini anachotaka kwako ni kumtumikia na kunyenyekea mbele zake.
Comments
Post a Comment