MAOMBI YA KUVUNJA VIFUNGO VILIVYOTUFUNGA NA VILIVYOTUZUNGUKA.




SOMO:


MAOMBI YA KUVUNJA VIFUNGO  VILIVYOTUFUNGA NA VILIVYOTUZUNGUKA.



Utangulizi.


Tunapokuwa  tumefunga  tunakuwa  tumemkaribia  MUNGU, katika kumkaribia  MUNGU tunakuwa  tunapeleka hoja zetu  na mahitaji  yetu  mbele za Bwana.

  Yakobo 4:8(a).  Mkaribieni Mungu naye  atawakaribia ninyi.

  Isaya  41:21.     Haya, Leteni maneno yenu asema BWANA; toeni hoja zenye         nguvu,asemamfalme wa Yakobo.

Isaya 43:26.   Unikumbushe, na tuhojiane; ELeza mambo yako,upate kupewa haki yako.

  • Tunapokuwa  tumemkaribia  Mungu, kwa kufunga   au  kwa  maombi MUNGU   anapendezwa  sana  na  sisi kutafuta  uso  wa BWANA, Lakini tunapofunga Mungu Anapenda  tufanye  yafuatayo;
  1. Kufungua  vifungo  vya  uovu.
          AINA  ZA VIFUNGO

   (a).   Uovu gani unakusumbua,
              Mfano; Umeua ,Umemtapeli mtu, Umemsingizia  mtu uongo akafungwa  jera, Unapendelea sana kutoa mimba,n.k.

Hivyo  vyoote  ni vifungo  vya  uovu  vinavyokuwa vimekufunga  mwana  wa MUNGU  kama  utakuwa  utenda  mojawapo  ya  mambo  hayo  yaliyotajwa  hapo  juu.


   (b).     Vifungo gani vinakutesaa.
                Mfano.   Ulevi, kujichua, uzinzi ,uasherati,kutembea na waume za watu/ wake za watu, kuvuta sigara/Bangi.


    (c).         Vifungo  vya magonjwa.  
                    Mfano,Kisukari,kansa, TB, Presha, Uvimbe wowote ule,n.k

 2.   Kuzilegeza kamba za nira    (Isaya  9:4)
       Nira  ni nini?      Ni kipande   cha  mti  afungwacho  ng`ombe  shingoni  au farasi  shingoni   anapolima  anapokokota  mzigo, kuvuta  mzigo.


        Maana nyingine ya nira ni kifaa ambacho  huvikwa  shingoni  mwa  Ng`ombe ,Punda,Farasi,au mnyama  mwingine  kwa  kusudi  la kuvuta  mzigo  nyuma  yake.

Nira uwa  na Lijamu   na  Hatamu  ili  kuweza  kumwongoza  mnyama  katika   njia  ambayo  Bwana   wake  amekusudia  kupita.


LIJAMU.  ni  kifaa ambacho  hufungwa  mdomoni .
HATAMU .Ni  kamba  ambazo  zimefungwa  kwenye  lijamu  ili  kumwongoza  mnyama  njia  apitayo.

KAMBA. Kamba ni  kitu chochote ambacho mtu ukitumia  kufunga  mizigo  inaweza kuwa manila, katani, waya mwepesi, n.k.


Hivyo  basi  mtu  wa MUNGU   nakuomba  uharibu  vitu  vifuatavyo  vinavyokuzunguka   katika  kufanya  hivyo,  kwa  kufanya  hivyo  itakufanya  kuwa  huru  maishani  mwako.


 -   Haribu  kamba za  mauti kwenye  maisha  yako , na kwenye  familia  yako zinazokuzunguka  Z aburi  18;4-5.

-         Haribu  kamba za kuzimu  zilizokuzunguka  
    Zaburi  18:4  Kamba za kuzimu  zilinizunguka, mitego ya mauti  ikanikabili .

-   Haribu kamba za wasio  haki walizokutamkia  usifanikwe.
     Wamekutamkia  usiolewe, usioe, usipate  kazi, usipate  watoto, watoto wako wawe wezi, wasifanikwe  n.k.


3. Kuwaacha  huru  walioonewa  na  Ibilisi.
      (a).  Kuna watu hawataki kabisaa kusikia  Injili  ikihubiriwa, wengine  ni WAKRISTO  wengine  ni madhehebu  Mengine.

Hao  wote  wameonewa na  Ibilisi wamefungwa  katika  fikra  zao wasiipokee INJILI  na kuponya  katika  maisha  yao  yote  sisi kaama  watumishi  wa YESU KRISTO   tunao  wajibu  kuhakikisha  woote  walioonewa  na  IBILISI  SHETANI   wanawekwa  huru  wanafunguliwaa.




Na mimi  nakutamkia  kwa  JINA LA  YESU  ALIYE  HAI  POKEA  UZIMA  KWA  JINA  LA YESU   mapepo yote  na  majini  yaliyojificha  kwenye  mwili  wakoo tookaa  kwa  JINA LA YESU  ALIYE  HAI.


NATAMKA   kufunguliwa  kwa jina  la YESU  aliye  hai  kama ni mizimu  ya KI-UKOO  na maagano  yote  ya kipepo  TOOKA  KWA  jina  LA YESU ALIYE HAI. Natamka  kufunguliwa  kuanzia  sasa  kwa  JINA LA YESU  SEMA  AMENI.


      (b).  Walioonewa  na  magonjwa  SUGU  kama  KISUKARI, KANSA, TB, PUMU, UVIMBE,  n,k.


Natamka   funguka  kwa  JINA  LA YESU  ALIYE  HAI  maana mwili  wa  mwanadamu  ni  hekalu la  Roho  mtakatifu  hivyo  IBILI SHETANI  hauna  nafasi  teena   katika  mwili  wa huyu mama/ huyu Baba/ Dada/ Kaka.Huyu mtoto.


Ninafuta  maagano  yote  ya  kipepo  KWA  JINA  LA YESU  ALIYE  HAI  maana  kila pando  asilolipanda  Baba  wa  mbinguni  litang`olewa  KWA  JINA  LA YESU  ALIE  HAI .


NAFUTA   maagano  yote  ya  KIPEPO  kwa  DAMU  YA  YESU  ALIYE  HAI , kuanzia  sasa  uwe  mzimaaa  Sema  AMEENI


KWA LEO  NAOMBA TUISHI  HAPO

Kama  haujampokea  YESU  KRISTO  AWE BWANA NA MWOKOZI  WA MAISHA  FUATISHA  SALA HII.

Sema   BWANA  YESU  ninakuja  kwako  mimi  ni mwenye  dhambi, ninatubu  dhambi  zangu zoote  nilizozitenda  kwa jujua  na kutokujua  nakili  nilitenda naomba  unisamehe  EE BYESU KRISTO ULIYE HAI  maana  imeandikwa  kwa  kupigwa  kwako  sisi  tumepona  na mimi   nakili  kupona klwa JINA LAKO YESU ULIYE HAI 

Naomba ulifute  jina  langu kwanye  kitabu  cha  ukumu  uliandike  ajaina langu  kwenye  kitabu  cha  uzima  kwakuwa  UFALME NI WAKO NA NGUVU  NA UTUKUFU  SASA  NA  HATA  MILELE  AMENI.


HONGERA SANA   mwana wa MUNGU  kwa KUOKOKA  tangia  leo umekuwa mwana  mpya USITENDE  DHAMBI TENA, MUNGU amekusamehe  dhambi zako na wala  hazikumbuki  teena.


Ni mimi  ndugu  yenu  katika KRISTO YESU
Baraka Audax
INJILI YA KRISTO ZANZIBAR
+255  717 46 1006


   WASILIANA NA MIMI  NIPATE KUKUTUMIA KITABU CHA HONGERA KWA KUOKOKA CHENYE MAFUNDISHO  YA AWALI YA KUUKULIA WOKOVU.


UBARIKIWE  SANA MWANA WA  MUNGU.
     


                                                             AMENI.

Comments

  1. Mbarikiwe sana wana MUNGU muwe na siku njema sana

    ReplyDelete
  2. Ok...

    What I'm going to tell you may sound kind of creepy, maybe even kind of "strange"

    HOW would you like it if you could simply press "Play" to listen to a short, "miracle tone"...

    And miraculously attract MORE MONEY to your LIFE?

    I'm talking about thousands... even MILLIONS of DOLLARS!

    Think it's too EASY? Think this couldn't possibly be for REAL??

    Well then, Let me tell you the news...

    Sometimes the most magical blessings in life are also the EASIEST!

    In fact, I'm going to provide you with PROOF by letting you listen to a REAL "magical money tone" I've synthesized...

    And do it FREE (no strings attached).

    You simply push "Play" and watch as your abundance angels fly into your life.. it starts right away..

    CLICK here NOW to play the marvelous "Miracle Abundance TONE" - it's my gift to you!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts