SOMO

UONAPO KUCHOKA NDIPO PALIPO NA SIRI YA MAFANIKIO YAKO.

Leo nataka nizungumzie  vitu  vitatu  ambavyo ni MIFUPA,MIKAVU na 

UPEPO.


 EZEKIEL 37:1-14. Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika  roho ya BWANA , akaniweka chini,katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; 2 akanipitisha  karibu nayo pande zote na tazama; palikuwa  na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.

Ukipata muda soma sura nzima lkn hapa nitazungumza kwa uchache sana.

MIFUPA: Ni ugumu wa jambo  au jaribu  ulilonalo  ambalo  linakusumbua.
MIKAVU: Kukata  tama, mtu  anapokuwa  katika  kipindi  kigumu  sana  cha  majaribu  makali  mtu  huyo huwa  haitaji  kufarijiwa  kama alivyozeaa  , mtu  huyo anahitaji sana  MUNGU amsaidie  sana na ROHO wa MUNGU amtie nguvu.

Mfano.


  • Ayubu  valipokuwa  katika  kipindi kigumu  cha majaribu hakutaka  kufarijiwa na mtu yoyote, wote waliokuwa  wanamfariji aliwaona kama upuuzi.
  • ELIFAZI  alipokuwa  anamtia  moyo  AYUBU alikuwa anamkataza  tu  yeye alitamani  sana BWANA  amuokoe.
  1. Mara nyingi  watu wanapokuwa  wanapita katika  hali ngumu ya maisha  yao  wanaweza baadhi yao kujikuta wanakunywa sumu, wanajinyonga, kujitupa baharini, kujigongesha kwenye magari, kujirusha kutoka  ghorofani n,k.
  2. Unapowaza  hayo  ndipo mara nyingi shetani anap[ata  nafasi kubwa ya kukutawala na kusababisha maafa makubwa lakini mara nyingi kama wewe ni MTUMISHI WA MUNGU,Ndipo Mungu anapoleta msaada maana MUNGU hapendi kuona watu wake wakiangamia. MUNGU analeta msaada wa kutokea  maana kila jambo/jaribu lijapo BWANA ANAFANYA NA MLANGO WA KUTOKEA.
EZEKIEL 37:7  Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii;palikuwa na mshindo mkuu; na tazama,tetemeko la nchi na ile mifupa ikasogeleana,mfupa kwa mfupa mwenziwe.

Mshindo mku; maana Mungu  anapotaka kukubariki huruhusu uwepo wake mahali ulipo.

MISHIPA: Mungu anapotaka kukurudishia  vile vitu vilivyopotea  uruhusu Baraka  hizo  ziwe  na ulinzi mkali.

Lazima  mara kwa mara umuulize MUNGU, Baraka  ulizo  nazo zimetokana  na yeye au siye yeye maana kama ni yeye na wewe itakubidi utembee  katika Baraka  zake na mafanikio yake/yako.




UPEPO: Ni uwepo wa Mungu ndani yake /yako lakini Mungu hajakutia pumzi,pindi anapokutia  pumzi kumbuka  unakuwa  mpya  na unabarikiwa zaidi ya mwanzo ulivyokuwa.

  1.   1.Kwa hiyo ndugu yangu yawezekana umepitia katika mateso magumu na shida nyingi sana umekauka  umeisha lakini jua kwamba Mungu anakuwazia mema sana na atakufanikisha mda si mrefu 
  2. Ndugu yangu Dada/ Mama/ KAKA kipindi hiki unachopitai najua ni kigumu sana likini MUNGU  anakuwazia sana mema kumbuka AYUBU  nayey alipitia kipindi  kigumu kama hiki lkn Hakuruhusu moyo wake kumwasi MUNGU wake na ndipo Mungu alimrudia na kumkumbuka , hata wewe atakukumbuka na kukurejea.
MWISHO. TAMKA USHINDI MARA ZAKO ZOOTE kwamba ninashinda kwa jina la Yesu maana katika yeye tuna shinda zaidi ya kushinda.


MBARIKIWE SANA WANA WA MUNGU
N i mimi ndugu yenu
BARAKA AUDAX
INJILI YA KRISTO ZANZIBAR
+255 717 461006

Comments

Popular Posts