SOMO:
MAOMBI YA KUFUTA LAANA ZINAZOTUFATILIA.
Utangulizi.
Laana ni maneno yanayotamkwa kinyume na Baraka,katika maisha ya mtu.
Mfano.
MAOMBI YA KUFUTA LAANA ZINAZOTUFATILIA.
Utangulizi.
Laana ni maneno yanayotamkwa kinyume na Baraka,katika maisha ya mtu.
Mfano.
- Yesu alipouendea mtini ili apate kula matunda yake alipoona hauna matunda aliulaani ukakaukaa mara moja. Marko 11:11-14.
- Na asubuhi yake wanafunzi walipopita kwenye ule mtini waliukata umenyauka Marko 11:20.
Laana inaweza kuwa ni ya maneno au kuwa ya kufanya wewe mwenyewe.
REUBENI : Alilala na Suria wa baba yake akajipatia laana kutoka kwa Baba yake YAKOBO, kipindi Yakobo anawabariki wanawe yeye hakumbariki bali alimlaani asiwe na UKUU WOWOTE.
Mwanzo 49:3-4. Hii ilikuwa laana ya REUBENI kujitengenezea yeye Mwenyewe na wapo Watu wengi mno ambao wamejitakia laana kwa kufanya weneywe kwa mikono yao wenyewe.
Mfano unakuta kijana anampiga mama yake mzazi au Baba yake mzazi ata kama mzazi amekukosea vipi hutakiwi kumpiga au kumnfokea yule ni Mzazi wako tu.
Watu wengine wanawasema watumishi wa MUNGU vibaya na kuwatukana kumbuka MIRIAMU na HARUNI walipoanza kumsema MUSA vibaya MUNGU alimuadhibu kwa UKOMA MIRIAMU
Mifano ya watu waliokuwa wamelaamiwa na jamaa zao.
NEHEMIA 13:1-3
Ukisoma HESABU sura ya 23,24 na 25 utamuona mfalme wa Moabu, akituma watu kwa Balaamu ili awalaani wana wa Israeli maana wana nguvu kumshinda kuliko yeye.
SABABU ZA KUFANYA HIVYO YAANI KUWALAANI WANA WA ISRAELI.
- Wana nguvu za kumshinda yeye.
- Aweza kupata kuwapiga
- Awafukuze watoke katika nchi yake ,
NI NINI CHA KUFANYA.
- Vunja laana zote ulizotamkiwa Mithali 18:20 na Mithali 26:2.
- Haribu na bomoa mapando yoote ya laana. Soma Mathayo 15:13 na Yeremia 1:10
- Yang`oe yote yanayokusibu kwa jina la YESU.
- Bomoa ufalme wote wa giza kwa Jina la YESU
- Haribu nguvu zote za shetani zinazokuwinda na kukutesa,
- Angamiza maajenti wote wa shetani waliotumwa waitese familia yako, kwenye uchumi wako, watoto wako, mifugo yako ,mazao yako, n.k WAANGAMIZE KWA JINA LA YESU NA MOTO WA YESU.
- Ijenge na kuipanda upyaa Madhabu ya BWANA shetani aliyokuwa ameivunja kwako, Jenga madhabahu ya BWANA Kwa kuizungushia Damu ya Yesu.
3.KRISTO ametukomboa katika laana zote tumia DAMU YA YESU kujitoa katika laana zote. Galatia 3:13
Mwisho Yawezekana Ukawa unapitia Kwenye Kipindi Kigumu Cha Matatizo Ya Kifamilia ninachokuomba Mwite YESU na iite DAMU YAKE IKUTAKASE
Kwa leo naishia hapa
ni mimi ndugu yako katika KRISTO
BARAKA AUDAX
INJILIO YA KRISTO ZANZIBAR
Whasap +255 717 461006
Comments
Post a Comment