Mwanzo 12:10-11
Kurithi ni
nini?. Kurithi ni kupokea kitu kutoka
mikononi mwa mtu mwingine ambacho
kilikuwa ni mali yake
mwenyewe na kumrithisha mtu mwingine.
MFANO:
Kupokea shamba ,Nyumba, Gari, Baiskeli n,k kutoka kwa mzazi wako/ mlezi wako na kukupa
wewe au mtu mwingine ambavyo tangu awali vilikuwa ni vya kwake yaani mali yake
mwenyewe anaamua kumpa/ kumkabithi mtu mwingine urithi wake.
·
IBRAHIMU alizaliwa na mzee Tera,baada ya gharika ya
NUHU,na baada ya kuzaliwa walikuwa wanaishi sehemu nmoja iitwayo URU WA WAKALDAYO.
·
Wakatoka uko wakaenda kaanani wakafika mpaka wa HARANI wakakaa huko.
·
BWANA alipomtokea IBRAHIMU alimwambia atoke katika nchi ile aende KAANANI na alipofika
KAANANI alitembelea katika miji kadha wa kadha lakini mwisho wa siku nchi ile ikaja kukumbwa
na njaa .
·
IBRAHIMU
akaamua kwenda uko MISRI kwa
ajili ya kutafuta chakula ale asije kufa kwa njaaa
IBRAHIMU.
1.
Alikumbwa na njaa katika nchi ya KAANANI akakimbilia MISRI.
2.
Alikuwa ni mwongo kwa ajili ya hofu.
Ø Alipoenda
MISRI alimwambia mke wake kuwa Wamisri wakikuuliza sema wewe ni dadangu kwakuwa wewe ni mzuri sana wa uso wasije
wakaniua mimi wakakuacha wewe uishi hai.
Ø Hapa tunaona
kwamba WIVU mtu unayempenda lazima utamuonea sana wivu kila wakati,Lakini
sasa wa IBRAHIMU ulipitiliza.
Ø IBRAHIMU alipoenda nchi ya kusini kwa wafilisti
alidnganya vile vile kwa hofu ile ile ya kuwa Yule sio mke wake bali ni dada yake.
v ABIMELEKI mfalme wa GERARI akatuma watu waende kumposaa
v Lakini
kwakuwa ABIMELEKI Mfalme wa GERARI
alikuwa ni mtu mkamilifu mbele za BWANA,
alikuwa akitenda mema na haki, mbele za BWANA, ndipo BWANA akamuonya katika
ndoto kuwa asitende dhambi Yule ni mke
wa mtu.
ü Tuwe wakamilifu mbele za BWANA ili BWANA atuokoe tusitende dhambi bila ya kujua.
ü Tukiwa wakamilifu mbele za BWANA atautpigania
sisi na wana wetu.
MATATIZO KADHAA YA KURITHI.
1.
IBRAHIMU mke wake alikuwa
ni tasa.Yaani SARA
2.
IBRAHIMU yeye alikuwa ni mwongo na muoga anadanganya huyu
sio mke wangu ni ndugu yangu ili asije akauwawa.
3.
IBRAHIMU alipatwa na Njaa 12:10.
4.
ISAKA mke wake naye alikuwa ni tasa kama
Baba yake 25:21 .
5.
NJAA Isaka naye alipitia kipindi kigumu kama cha BABA
yake katika nchi yao wenyewe walipokuwa wanaishi nchi ya GERARI.
6.
ISAKA akadanganya kama BABA yake
kwamba REBEKA ni ndugu yake katika nchi ya GERARI. 26:6
ü Matatizo
hayo ya kurithi yaliendelea kwenye familia ya mzee IBRAHIMU hadi kwa mjukuu wake Yakobo.
ü Yakobo alioa wake wawili mkubwa ni
RAHELI na Mdogo
ni LEA .
ü LEA alikuwa
tasa hazai lakini
RAHELI alikuwa na watoto.
7.
ROHO za chuki kuchukiana na hiyo ilianzia kwa
SARA na HAJIRI wake za IBRAHIMU mpaka
kwa wake za YAKOBO na watoto wao.
Ø Yusufu
alipokuwa akichunga kondoo na ndugu zaake
wana wa BILHA na ZILPA Vijakazi wa
LEA na RAHELI walimchukia saana YUSUFU .
Ø Walimchukia sana YUSUFU
Kiasi kwamba wakaazimia kumuua ili maono yake na ndoto zake zisitimie.
Ø Lakini
piaa waliposhindwaa wakaamua kumuuza ndugu yao
kwa vipande 20 vya fedha na
kusingizia ameraluriwa na mnyama mkali .
YAKOBO.
1) Alikuwa ni mjukuu wa IBRAHIMU , alipitia katika kipindi kigumu sana kama
cha BABU yake na BABA yake ya NJAA na
UTASA.
2) Mke wake
YAKOBO alikuwa tasa hazai ,
3) YAKOBO
alipatwa na njaa kubwa katika
taifa lao la KAANANI walilokuwa wanaishi wenyewe , kaama BABU yake na BABA yake
walivyopatwa na njaa.
Wakati mwingine sisi kama wanadamu tunapitia katika wakati mgumu sana wa maisha bila ya kujua vyanzo vyake vimesababishwa na nini na kipi tufanye lkn ni matumaini yangu kuwa leo umejifunza namna ya kuvishughurikia vyanzo vya matatizo yako ya kiuchumi uliyonayo.
Ni mimi ndugu yenu katika KRISTO YESU
BARAKA AUDAX
INJILI YA KRISTO ZANZIBAR
Ni mimi ndugu yenu katika KRISTO YESU
BARAKA AUDAX
INJILI YA KRISTO ZANZIBAR
+255 717 461006
Comments
Post a Comment