MPE BWANA KIPAUMBELE KATIKA KUMTUMIKIA.

                                        BWANA  YESU  ASIFIWE.



Karibu  tujifunze  somo  zuri  liitwalo 
MPE  BWANA KIPAUMBELE  KATIKA KUMTUMIKIA.


 Sisi  tuliokoka  tunakuwa  walimu  wa  Yesu  Kristo
Maana  BWANA  YESU  ametuchagua  tuhihubiri  injili  yake  KRISTO.                       
Marko  16:15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.
20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.

Kwa  hiyo  maandiko  haya  yanatuonesha  kuwa   wewe  uliyeokoka  hata  kama  unao  udhaifu  wa  aina  yoyote  hile  TUNATAKIWA  KUIHUBIRI   IJILI  YA  BWANA  YESU  KRISTO.Bila  kujali  hali  yoyote  tunayopitia   yawezekana  upo  katika  nchi  ambayo  Wakiristo  wana  chinjwa  na kuuwawa   unafikilia  utahubirije  swala  moja  ninalokutia  moyo  hubiri  tu  hata  kwenye  mtandao  wapo  watakao  soma  na  wengine  watapuuza  na  kuacha  tu.

               MAMBO  MAKUU  KATIKA  KUMPA  BWANA  KIPAUMBELE.

1.UAMINIFU:                                                                                                                                            Katika  kumtumikia  Bwana  tunatakiwa  kuwa  sana  waaminifu  kwa  kila  kazi  ya MUNGU  tunayoifanya  kama  wewe  ni  mwanakwaya  unatakiwa  kuwa  mwaminifu  katika  kumwimbia  MUNGU, Kama  wewe  ni  Shemasi, Mzee  wa  kanisa, Katibu,  Mwekazina, n.k unatakiwa  kuwa  mwaminifu.

               Watu  wengine  uwa  wanafikiria  kwamba  kwakuwa  wao  sio  viongozi  wa  kanisa  mahali  fulani  basi  haiwapasi  kumtumikia   MUNGU, Hapana   kwa  sehemu  yoyote  uliyopo  ata  kama  unafagia  kanisa, unapanga  viti , au  unafagia  chooni , au unadili  na  Bustani, Parking, fundi  vyombo, n,k   fanya  kwa  uaminifu  kazi  yako  maana  siku  za  mwisho  kazi  yako  itapimwa.  IKor.4:2

2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.

2.KUJIDHABIU/ KUJITOWA  KWA  BWANA.

Warumi  12:2-7

 Hapa  tunapata  kuona   Mariamu  alijidhabiu  alijitowa  kwa  BWANA  bila  kuangalia  kuwa  hiyo  NARDO  ingeuzwa  bei  gani  ili  apate  pesa  kwa  ajili  ya  matumizi  yake  binafsi.



4.MUDA.

Kama  umejitowa  kumtumikia   BWANA  ni  lazima  kwako  kuzingatia  sana  muda.Maana  zama  hizi  ni  zama  za  uovu  na  shetani  anajua  kukutumia  sana  kwa  kutuharibia 
 muda  bila  hata  kusoma  Biblia  na  hata  kuyachambua  maandiko.

Ebrania  11:15-16

15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.


Nina  imani  utakuwa  umebarikiwa  kwa  leo  wacha  tuishie  hapo  tutaendelea  wakati  mwingine  sehemu  ya  pili.

Barikiwa  sana  wapendwa  katika  Kristo
Ni  mimi  ndugu  yako  Baraka  Audax
Injili  ya  Kristo  Zanzibar  Tanzania
0717  46  1006 










Comments

Popular Posts