SHEREHE YA WAMAMA ZANZIBAR YAWABARIKI MAELFU YA WATU
SHEREHE YA WAMAMA
YAWABARIKI MAELFU YA WATU ZANZIBAR.Sherehe wa wamama wa kanisa la PENTECOSTE ASSEMBLY OD GOD ZANZIBAR (P A G} iliyofanyika leo jumapili imewagusa watu wengi na kuwabariki maelfu ya watu walio hudhuria kanisani hapo.
Kanisa la PENTECOSTE ASSEMBLY OD GOD TANZANIA,Lilijiwekea utaratibu mzuri wa kuwa kwa kila mwaka kunakuwepo sherehe mbali mbali ya vijana na sherahe ya wamama, ivo mnamo wiki hii ilikuwa ndo sherehe ya wamama kwakweli ilikuwa ni sherehe kubwa mno na nzuri sana ambayo iliwabariki maelfu ya watu waliofika kanisani na wageni waliofika hapo kanisani.
Ninaamini utakuwa umebarikiwa sana Injili ya Kristo Zanzibar tutazidi kukuabarisha mengi.
Mnamo Juma pili ya leo ilikuwa ni
sherehe ya wamama,ambayo
ilianza toka asubuhi
mpaka saa nane mchana,Shere hiyo iliudhuliwa na
watu mbali mbali kutoka
madhehebu mbali mbali na tofauti tofauti.
1:Picha hiyo
hapo juu inawanesha
baadhi ya wamama wachache wakiwa wana cheza
igizo lililobeba ujumbe wa Mwanamke kumjali mume wake ilikuruhusu nguvu
za BWANA zitawale familia nzima
2:Picha hiyo
hapo juu ni moja
ya wamama waliokuwa wanamsikiliza muhubiri
aliyekuwa naigiza namna
ya kuwafundisha kushuhudia
nyumba kwa nyumba.
3:Picha
inayofuata hapo chini ni baada ya kuwa
wapimepita mtaani kushuhudia
watu walikubali kuokoka
na kumpokea BWANA YESU awe ni BWANA na
mwokozi wa maisha yao,
Pamoja na
wamama kuandaa sherehe
kubwa pia waliwza
kuandaa nyimbo mbali mbali ,Vyakula pamoja
na vinywaji vya
kutosha kanisa zima.
4:Picha
hiyo hapo chini ni moja
ya kwaya ya wamama
wakimtukuza MUNGU.Wakiimba wimbo
ulio kuwa na
ujumbe wa Mwanamke
ndiye MLEZI WA FAMILIA.Hivo inampasa
kuwa na hekima,Busara, Ufahamu,
Upendo na adabu kwa mume
wake na majirani zake
wote wanaomzunguka.
5:Aliyejifunga kanga
kwa picha za hapo chini mbele
ni mama Mchungaji
wakiwa wana mwimbia BWANA
nyimbo za sifa.Zilizo
jaa shangwe nyingi
na nderemo, vigeregere na vifijo. Akika siku
hiyo ilikuwa ni
siku ya kipekee
sana na imeacha
historia kubwa mno
kwa maana ni
mengi sana na mazuri
mno wamama waliyoyafanya .Na kuzigusa mioyo
ya watu wengi kwakuwa
mtu yoyote yule
akifanya jambo zuri
nilazima atasifiwa na kusemewa
mazuri.
Wamama
mnastahiri pongezi na
hongereni sana na MUNGU
wa mbingunu awabariki
sana.
Pamoja na zawadi
nyingi na nzuri walizo mpa Mchungaji AMOSI wa
kanisa hilo hawakusahu kumpa
pole na hongera kwa
kazi nzito ya kueneza Injili
visiwani Zanzibar kwa kumpa fedha taslimu laki
mbili kama sehemu kumshukuru kwa
kazi nzuri anayofanya .
Kama mnavojua kazi ya kuhubiri
Injili ya Kristo Zanzibar
imekuwa na changamoto
nyingi mno lakini
changamoto hizo haziwazuhii wachungaji kuendelea
kumuhubiri KRISTO.
6:Picha hiyo hapo ni Mchungaji AMOSI wa Kanisa hilo
la PENTECOSTE akiwa anatabasamu
kwa mambo makubwa ya wamama
waliyomfanyia kwenye sherehe
yao.
Comments
Post a Comment