MCHUNGAJI AFUNGWA JERA KISA NI UPAKO WA SAUTI KUBWA
MCHUNGAJI AFUNGWA JELA KWA SABABU YA SAUTI KUBWA YA VYOMBO VYA MZIKI KANISANI KWAKE.
Mchungaji Johnnie Clark |
Mchungaji Johnnie Clark na mkewe Harriet Clark |
Kwa upande wa mke wa mchungaji huyo Harriet Clark amekiambia kituo hicho kwamba haamini kilichotokea kwa mumewe kufungwa kwa kosa la kumtumikia Mungu, baada ya hili nini kinafuata sasa? ni juu yao majirani kusema kama wanabugudhiwa na sauti ama la, alimalizia mchungaji Herriet.
Kutokana na tatizo hilo jaji ameamuru kanisa hilo kutotumia ngoma (drums), vipaza sauti kati ya saa 2 usiku na saa 2 asubuhi ikiwa ni adhabu ya miaka miwili. Kwa upande wa mmoja wa majirani na muumini wa kanisa hilo kijana Thomas Borders(20) amesema unaweza kuchukua mashine ya kukatia nyasi na kwenda nje kuifanyia kazi hata kama kuna mtu atalalamika lakini hakuna hatua itakayochukuliwa, lakini inapokuja suala la kumwabudu Mungu ni tatizo.
Viongozi wa kanisa hilo wamedai kanisa limekuwepo kwa muda mrefu katika eneo hilo hata kabla ya kuwepo kwa nyumba za majirani hao na kwamba kanisa halitakiwa kuadhibiwa kwa ajili ya hilo. Njia kuu ya kutibu tatizo hilo ni kwa mchungaji Clark kuweka vifaa vya kuzuia sauti kutoka nje (sound proof) kitu ambacho hata hivyo si rahisi kwakuwa ni bei kubwa .
Lakini pamoja na matukio hayo bado waumini wake wanaendelea kumwabudu na kumtukuza Mungu kwani imeandikwa kuwaogopa wanadamu huleta mitego.
Comments
Post a Comment