MCHAWI ADONDOKA KANISANI WAKATI WA MAOMBI:
MTAZAME MCHAWI ALIVYODONDOKA KANISANI.
NIkweli imetokea! Tukio hilo limetokea kwenye Kanisa la Paradise Internation
Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani)
anayedaiwa mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi
kutembea.
Mwanamke anayedaiwa kuwa mchawi akiwa amedondoka Kanisani.
Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa wamezama kwenye maombi ya kufunga.
Ilidaiwa kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maombi
hayo, Nabii Gideon Parapanda aliwahakikishia kuwa usiku huo kutatokea
mambo ya ajabu kufuatia maombi hayo.
Inadaiwa ilipofika saa saba usiku mwanamke huyo akiwa na
wenzake watatu, walidondokea kanisani hapo na kusababisha taharuki kwa
waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani. Mwanamke huyo alikuwa na
kitambaa chekundu kikidaiwa ni hirizi, fimbo nyeusi iliyozungushiwa
shanga na alikuwa amejipaka masizi mwilini.
Mwanamke baada ya kudondokea kanisani na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani.
Akizungumza na Uwazi, Nabii Parapanda alisema watu hao
walidondoka watatu, wawili walifanikiwa kukimbia akabaki huyo mmoja
aliyejitambulishwa kwa jina moja la Aisha, mkazi wa Mwananyamala A
jijini Dar.
Baada ya tukio hilo vyombo vya ulinzi, askari wa JWTZ na
polisi walifika kwa lengo la kuhakikisha usalama wa eneo hilo lakini
nabii huyo aliomba mtu huyo asichukuliwe hadi atapofanyiwa maombi
maalum.
Ombi la kiongozi huyo lilikubaliwa ambapo Aisha
alipandishwa madhabahuni na kukiri kuwa alikuwa na wenzake watano
lakini katika kuanguka walikuwa watatu, wawili walifanikiwa kukimbia
bila kusema walikuwa wakitoka wapi kwenda wapi.
Kitambaa chekundu alichokuwa nacho mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado yuko kanisani hapo kwa maombi.”
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado yuko kanisani hapo kwa maombi.”
BARIKIWA SANA MTU WA MUNGU
BARAKA AUDAX
0717-461006
INJIRI YA KRISTO ZANZIBAR
Comments
Post a Comment