USHINDI DHIDI YA LAANA.

KARIBU  TUJIFUNZE  SOMO  HILI:     

                                                                                                                                                       USHINDI  DHIDI  YA  LAANA.                                                                                                 
Laana ni maneno  mabaya  yanayotamkwa  kutoka  kinywani mwa mtu  au vinywani  mwa  watu  kwa  nia mbaya ya  kukutakia jambo  la  kukudhulu  katika  maisha  yako  ya  baadae.            

Mtu  mwenye  laana  ni   yule anayekwenda  kinyume  na  maagizo  aidha  ya  wazazi  wake  au  ndugu  zake, au  kwa Mungu  wake.


Laana inaambatana  na  matamko  ya maneno  ambayo  si  mazuri  katika maisha  yako.



Torati  11:28 

Na  laana ni  hapo  msiposikiza  maagizo  ya BWANA, Mungu  wenu,mkikengeuka  katika  njia  niwaagizayo  leo,kwa  kuandama  miungu  mingine   msiyoijua.


Hapa  tunaona  kuwa  Musa  alikuwa  akiwapa maagizo  ya  Mungu  aliyopewa, kwa wana  wa  Israel  na alikuwa  akiwasisitiza  kuwa  wasipo  enda  katika  maagizo  ya  BWANA  laana  itakuwa  juu   yao.


Na  ndivo  inavokuwa  kwa  wana  wa  Mungu   ambao  ndo wewe  na  mimi, wanapokuwa  watu  wametutamkia  maneno  ya  laana  tunapaswa  kuyabatilisha  na  kuyafanya  baraka.


Zaburi   33 :10 
Bwana  huyabatirisha  mashauri  ya mataifa, Huyatangua   makusudi  ya  watu.

Ndugu  yangu  mtu  wa  Mungu  nakushauri  leo  usomapo  ujumbe   huu  batilisha  makusudi  ya  mataifa  waliyokutamkia  na  kukulaani  usifanikiwe.



  1. Tamka  kwa  kumaanisha  kuwa  nakataa  laana  walizo  nitamkia  katika  maisha  yangu,Zivunje  kwa  kutumia   damu  ya  Yesu  Kristo  aliye  hai.
  2.  Katika   Zaburi  34:17: Neno  la  BWANA  linasema  walilia,  naye  Bwana  akawasikia,akawaponya  na  taabu  zao  naamini  kama  utakuwa  umetamikwwa  laana  ukimlilia  BWANA  AKIKA  ATAKUPONYA: 
Kwa  leo  naomba  tuishie  hapo  tutaendelea  wakati  mwingine

Barikiwa  sana  naamini  Mungu  atakuponya  jeraha  zako  na kukuweka  huru,


Picha hii  ni  moja  ya  waimbaji  walio  udhulia  katika  vipidi  vyetu  vya  mafundisho  na  masomo  yetu  ambayo  Mungu  amenipatia  kibali  kuyafundisha.


Ni mimi  ndugu  yako
Baraka Audax
Injili  ya  Kristo  zanzibar
0717  461006.

Comments

Popular Posts