JIHADHARI NA MANENO YA WANADAMU.
SOMO: : JIHADHALI NA MANENO YA WANADAMU:
Somo letu la leo tunakwenda kujifunza kuhusu kujihadhari na wanadamu:
Unapokuwa katika kipindi kigumu cha maisha ambacho ni kipindi cha mpito watu wengi sana wanaweza kukushambulia kwa maneno na kukusababishia maumivu mengi moyoni.
Ayubu 2:
Hapo tunaona kuwa pamoja na kufanikiwa kimaendeleo na uchumi mzuri aliokuwa nao AYUBU, lakini bado shetani alikuwa anamuwinda kwa nguvu kwa kumchongea sana mbele za Mungu ila Mungu hakumuruhusu.
Ayubu 2:3(e) Ujapokuwa ulinichochea juua yake, ili nimwangwamize pasipokuwa na sababu.
Ndivo ilivo kwa sisi wana wa Mungu kwamba tunaweza kuwa tunapitia katika mazingira magumu lakini pamoja na hao kama Mungu bado hajaruhusu uhangamie bado atazidi kukulinda tu.
MANENO YA WANADAMU:
Unapokuwa unapitia katika kipindi hicho kigumu bado wanadamu wanazidi kukuhandama sana ila kumbuka sana usije ruhusu mpenyo wa kipepo ukakuharibia maisha yako, na mpenyo huo ni kama kujibizana nao vibaya wanaokutamkia vibaya na kukudharau saa nyingine wanakutukana kutokana na kipato cha maisha yako kilivo kwa sasa ila naamini kuwa Mungu aliyekuumba hawezi kukuacha kabisa uhangamie.
MFANO: Ayubu 2:9
Ndipo mkewe akamwambia, je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Ukamkufuru MUNGU ukafe.
Hapo tumeona mkewe Ayubu ndo anakuwa wa kwanza kumwambia maneno ya maudhi, yawezekana wanafunzi wenzako wakawa wanakwambia maneno ya maudhi na kukudharau kwa ajili ya kipato au kushuka kwako darasani napenda nikwambie muangalie Bwana aliyekuumba na mlilie yeye peke yake wasikushughulishe hao.
Yawezekana wapangaji wenzako wakakuinukia na kukwambia maneno yasiyofaa ya kejeli na maudhi usiwaangalie na kuanza kujibizana nao maneno wala usimjibu mpunbavu sawa aswa na upumbavu wake usije ukafanana naye.
Siku moja nilikuwa mahali fulani nikiwa nimeharikwa na mpendwa mmoja nyumbani nikiwa pamoja na watumishi wenzangu nikasikia wanawake wa mle ndani wakimjadili mwenzao aliyekuwa anapika dagaa na kumtolea maneno ya dhihaka nyingi mno. Tumechoshwa na harufu ya misumari humu ndani misumari yenyewe inachoma kabla haujaila sasa ukiiweka tumboni itakuwaje.
Nilipowafuata na kuwahubiri injili ya BWANA walitubu dhambi zao na kujiona kuwa walichokuwa wanafanya sio haki mbele za Mungu ivyo maneno ya wanadamu wasikusababishe kukutoa katika mpango wa BWANA maana yeye anajua mawazo anayokuwazaia katika maisha yako ya baadae'
Hakika naamini utakuwa umebarikwa sana usiache kuomba wala kumtumikia Bwana katika maisha yako,barikiwa sana mtu wa Mungu.
Ni mimi ndugu yako,
BARAKA AUDAX
Injili ya Kristo Zanzibar
0717 461006
Barikiwa sana.

Comments
Post a Comment