KUMSHUKURU MUNGU NI LAZIMA
BWANA YESU asifiwe rafiki popote ulipo,
Nakukaribisha tujifunze kuhusu kumshukuru MUNGU
na faida zake.
Mfano wewe ni Baba/Mama na una watoto wako ambao
mara kwa mara huwa unawaletea zawadi lakini katika hao mmoja hukushukuru kila
ukimpa zawadi na mwingine hana habari na kukushukuru na kila mara unawaletea
zawadi, je ni yupi kati ya hao watoto wako ambaye utapenda kumletea zawadi kila
siku? Ukweli ni kwamba yule anayethamini zawadi yako kwa kukushukuru kila siku
ndio utakuwa unatamani kumletea zawadi kila siku. Na kwa MUNGU ni hivyo wale
wanaorudisha shukrani huwathamini zaidi kuliko wasio na shukrani. Ndugu
kushukuru ni muhimu sana na kama huna utaratibu wa kumshukuru MUNGU anza leo
tena kila ukiomba au kupokea toka kwake shukuru ndugu.
-Kwa wateule kumshukuru MUNGU ni jambo la lazima maana kufanya hivyo inaonyesha kwamba ulimtegemea MUNGU na ulihitaji msaada wake na bado unaamini hata kwa yale unayotarajia au hujapokea, utapokea muda mfupi ujao.
-Kumshukuru MUNGU ni kurudisha shukrani kwake kwa fadhili alizokutendea.
-Kumshukuru MUNGU ni kuthibitisha kwamba MUNGU anaweza kukutendea muujiza hata kwa yale ambayo bado hujapokea yaani kwa imani unaamini utapokea na kwa kweli tendo hili ni tendo la imani sana yaani unakuwa na uhakika kwamba utapokea tu hata iweje.
-Kumshukuru MUNGU ni kumwonyesha shetani na adui
zako wote kwamba MUNGU ndiye msaada wako na atakushindia.
-Kumshukuru MUNGU ni kuonyesha kwamba kiwango chako cha imani kwa YESU KRISTO ni kikubwa sana maana una uhakika kwamba amekutendea tayari na bado atakutendea tena na tena. Ni tendo la imani kwamba jambo hilo uliloomba kwa MUNGU tayari limetendeka kwenye ulimwengu wa roho na sasa bado kidogo tu litatimia kwenye ulimwengu wa mwili.
-Kumshukuru MUNGU ni kuonyesha kwamba shetani
ameshindwa kwako.
-Kumshukuru MUNGU ni kumwaibisha shetani na
malaika zake.
MUNGU akupe ufahamu wa kumshukuru siku zote
katika jina la YESU KRISTO.
Katika Zaburi 9:1-2 inasema ‘’Nitamshukuru BWANA
kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yake yote ya ajabu. Nitafurahi na
kukushangilia wewe; Nitaliimba jina lako wewe uliye juu” Mtumishi wa MUNGU hapa
anasema atamshukuru MUNGU siku zote yaani siku zote za mwaka na haya ndiyo
yanatakiwa yafanywe na wewe ndugu yangu
unayesoma ujumbe huu, na mimi naamini kila mtu ana sababu ya kumshukuru
MUNGU siku zote maana pumzi na uzima aliokupa MUNGU ni zawadi ambayo lazima
umshukuru MUNGU kila siku maadamu uko hai maana ni kwa neema yake,
Ndugu uwe katika imani na matendo ambayo yanasema
‘’MUNGU ananionaje na sio kwamba watu
wananionaje’’.
Ukimwangalia MUNGU utamshukuru kila saa lakini
ukiwaangalia wanadamu utashindwa kumpa
MUNGU utukufu wake kwa kumshukuru. Liko tatizo kwa watu wengi na hata tatizo
hili lipo hadi kwa baadhi ya wahubiri mfano wakati wa ibada ya maombi kipindi
ambacho kanisa linatakiwa liombe rehema kwa MUNGU na kumshukuru MUNGU ndio
wakati wa mchungaji au Nabii au Mtume kuomba bila kutumia Mic au kuomba kwa
sauti ya chini chini kwa sababu ya kuwatazama wanadamu badala ya kumtazama
MUNGU. Mtumishi mwenzangu katika KRISTO naomba tumpe MUNGU utukufu wote sio
tunaomba kwa sauti wakati tu tunaomba MUNGU atuinue kihuduma lakini wakati wa
kutubu na kumshukuru MUNGU tunazima mic na kuomba kwa sauti ya chini sana.
Ndugu yangu kushukuru MUNGU ni jambo ambalo hata BWANA YESU alitufundisha
mfano angalia Mathayo 5:11-12(Heri ninyi watakaowashutumu na kuwaudhi na
kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia kwa
kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa
kabla yenu’’ Ndugu ni vizuri kusema ‘’Asante BABA wa mbinguni’’ hata kama unapitia kwenye hali ngumu ila weka
imani kwamba MUNGU yuko pamoja na wewe na muujiza wako uko karibu sana.
BWANA YESU anatutaka tushukuru kwa kushangalia na
kufurahi.
Hana aliomba maombi ya shukrani baada ya kupata
mtoto Samweli na MUNGU baada ya maombi hayo ya kushukuru ya Hana alimpa watoto
wengine watano(5) hii iko 1 Samweli 2:1,2,10,21.(Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu
imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa
kuwa naufurahia wokovu wako;
Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama MUNGU wetu....... Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu miisho ya dunia......Naye BWANA akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, wa
kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za
BWANA.
)
-Ndugu mshukuru MUNGU kwa hicho kimoja alichokupa ili azione shukrani zako na kukupa vingine 5 kama alivyofanya kwa Hana. Lakini kama tukiwa hatuna shukrani kwa MUNGU tunaweza hata kunyang’anywa hata hicho kimoja tulichonacho.
Katika 2 Nyakati 20:21(Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele. ) ni mambo ya kumshukuru MUNGU pia katika Zaburi 107:1(Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.), Zaburi 118:21 pia katika Isaya 12:4.
BWANA YESU alishukuru hata kabla ya kupokea kutoka kwa BABA yake iko Mathayo 26:27.
-Ndugu mshukuru MUNGU kwa hicho kimoja alichokupa ili azione shukrani zako na kukupa vingine 5 kama alivyofanya kwa Hana. Lakini kama tukiwa hatuna shukrani kwa MUNGU tunaweza hata kunyang’anywa hata hicho kimoja tulichonacho.
Katika 2 Nyakati 20:21(Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele. ) ni mambo ya kumshukuru MUNGU pia katika Zaburi 107:1(Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.), Zaburi 118:21 pia katika Isaya 12:4.
BWANA YESU alishukuru hata kabla ya kupokea kutoka kwa BABA yake iko Mathayo 26:27.
Katika Warumi 14:9 pia katika 1 Kor 15:57 Hii
inaonyesha kumshukuru MUNGU ni jambo la lazima kwa wateule wake KRISTO.
-Ndugu shukuru hata kwa ajili ya wengine, shukuru
kwa ajili ya mmeo/mkeo ambaye MUNGU amekupa, shukuru kwa ajili ya Watoto wako
ambao MUNGU amekupa, shukuru kwa ajili ya mchungaji wako, Mama yako ,Baba yako,
kiongozi wako na hata kazi yako ambayo MUNGU amekupa.
Waefeso 1:16 inatufundisha kumshukuru sana MUNGU
maana kwa kuonyesha shukrani ndio kuendelea kupokea zaidi.
Tunatakiwa kumshukuru MUNGU bila kukoma 1
Thesalonike 2:13 pia 1 Thesalonike 5:16:22. Na wakolosai 1:3.
Tudumu katika kuomba huku tukimshukuru MUNGU kila
iitwapo leo. Wakolosai 4:2.
Maombi
Asante BABA wa mbinguni kwa somo hili
linalonijurisha kwamba nimepokea kutoka kwako na pia nitapokea zaidi kutoka
kwako baada ya mimi kuwa mtu wa kukushukuru . Asante BWANA kwa uzima wa milele
ulionipa kupitia Mwanao YESU KRISTO, Hakika unastahili kushukuriwa MUNGU siku
zote na miaka yote, unayenilinda ushukuriwe milele katika jina la YESU KRISTO.
Amen.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
BARAKA AUDAX
0717 461006
INJILI YA KRISTO ZANZIBAR
BARIKIWA SANA.
BARAKA AUDAX
0717 461006
INJILI YA KRISTO ZANZIBAR
BARIKIWA SANA.
Comments
Post a Comment