SOMO:

                      MAOMBI YA KUFUTA LAANA ZINAZOTUFATILIA.
Utangulizi.
Laana ni maneno yanayotamkwa kinyume na Baraka,katika maisha ya mtu.

Mfano.


  • Yesu  alipouendea  mtini ili apate kula  matunda  yake alipoona hauna matunda  aliulaani ukakaukaa mara moja.  Marko 11:11-14.  
  • Na asubuhi yake  wanafunzi  walipopita  kwenye  ule mtini waliukata   umenyauka  Marko 11:20.
Laana inaweza kuwa ni ya maneno au kuwa ya kufanya wewe mwenyewe.

REUBENI : Alilala  na Suria  wa baba  yake  akajipatia  laana kutoka  kwa  Baba yake YAKOBO, kipindi Yakobo  anawabariki  wanawe  yeye hakumbariki bali  alimlaani  asiwe  na UKUU WOWOTE.

  Mwanzo 49:3-4.  Hii  ilikuwa laana ya REUBENI kujitengenezea  yeye  Mwenyewe  na wapo Watu wengi mno ambao wamejitakia laana kwa kufanya weneywe kwa mikono yao wenyewe.

Mfano unakuta  kijana anampiga mama yake mzazi au Baba yake mzazi ata kama mzazi amekukosea  vipi  hutakiwi  kumpiga  au kumnfokea  yule ni  Mzazi wako tu.

Watu  wengine  wanawasema  watumishi wa  MUNGU  vibaya na kuwatukana  kumbuka  MIRIAMU na HARUNI   walipoanza  kumsema MUSA vibaya  MUNGU  alimuadhibu  kwa UKOMA MIRIAMU

Mifano ya watu waliokuwa wamelaamiwa na jamaa zao.
NEHEMIA 13:1-3  

Ukisoma  HESABU sura ya 23,24 na 25  utamuona  mfalme wa Moabu, akituma  watu  kwa  Balaamu  ili awalaani wana wa Israeli maana wana nguvu  kumshinda kuliko yeye. 


SABABU ZA KUFANYA HIVYO YAANI KUWALAANI WANA WA ISRAELI.

  1. Wana   nguvu za kumshinda yeye.
  2. Aweza  kupata kuwapiga 
  3. Awafukuze watoke  katika  nchi yake ,
NI  NINI CHA  KUFANYA.
  1. Vunja   laana zote ulizotamkiwa   Mithali  18:20   na  Mithali  26:2.
  2. Haribu na bomoa  mapando yoote ya laana.                                                                                 Soma  Mathayo  15:13  na    Yeremia 1:10
  •  Yang`oe  yote yanayokusibu kwa jina la YESU.
  • Bomoa  ufalme wote wa giza  kwa Jina  la YESU
  • Haribu  nguvu zote za shetani zinazokuwinda  na  kukutesa,
  • Angamiza  maajenti  wote wa  shetani  waliotumwa  waitese  familia  yako, kwenye  uchumi wako, watoto wako,  mifugo yako ,mazao yako,  n.k WAANGAMIZE KWA JINA LA YESU NA MOTO WA YESU.
  • Ijenge  na  kuipanda  upyaa Madhabu  ya BWANA  shetani aliyokuwa  ameivunja  kwako, Jenga  madhabahu  ya  BWANA Kwa kuizungushia  Damu ya Yesu.
   3.KRISTO ametukomboa  katika  laana zote  tumia DAMU YA YESU  kujitoa katika laana zote. Galatia    3:13 



Mwisho  Yawezekana Ukawa unapitia Kwenye Kipindi Kigumu Cha Matatizo Ya Kifamilia  ninachokuomba Mwite YESU na iite DAMU YAKE IKUTAKASE


Kwa leo naishia hapa 
ni mimi ndugu yako katika KRISTO
BARAKA AUDAX
INJILIO YA KRISTO ZANZIBAR
Whasap  +255 717 461006



Comments

Popular Posts