WATEULE WA YESU TUKAZE MWENDO.

              


karibu mpendwa tujifunze somo hili muhimu kwa maisha ya waende mbinguni.

Ukristo ni safari.
Mtu anapotubu dhambi na kumpokea YESU KRISTO kwa imani awe ni BWANA na MWOKOZI wake,  huwa ameanza safari.
Safari hii ni kwenda mbinguni, kule mbinguni anakuwa amewekewa taji ya uzima. Taji hii ataipokea siku ya mwisho wakati wa hukumu ya watu yetu na kumbuka kuwa siku hiyo BWANA YESU atawabagua au kuwatenga mbuzi na kondoo, hao mbuzi ni wale waliokataa kumpokea yeye na hao kondoo ni wateule wa MUNGU waliompa maisha yao BWANA YESU na waliishi katika yeye siku zote, yaani walioshinda ulimwengu  na tamaa zake.

Sote ambao tumemwamini BWANA YESU, tunajua safari hii ilivyo ngumu na ndefu, ina vikwazo vingi na magumu mengi. Sisi kwa vile tunaujua utamu wa kuishi ndani ya KRISTO, hatutaki wala hatuwezi kumwacha. Tunatamani sana siku  yetu ya kufa  ikifika , kama tukijua basi tuseme kama mtume Paulo ‘’…..wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza , imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo BWANA , mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile…’’ -2 Timotheo 4:6-8.

Lakini tunafahamu pia kwamba wako wenzetu tunaowafahamu , ambao waliamini na kumpokea YESU kama sisi, wakaanza safari ; baadae wakarudi nyuma na kuanguka. Hili linatisha sana, je sisi tunaweza kushindwa kama wao? . Kweli tunaweza kukutana na vikwazo tukakata tamaa: au tukaishi maisha ya kiroho  baadae tukachoka; au tukazimia njiani. Ingawa tunajua tumewekewa taji ya haki, taji hii ni kwa wale tu watakaoshinda. Ndugu tujitahidi kusonga mbele maana ushindi katika jina la YESU upo na pia ni faida kuu kuliko zote kama tukishinda. BWANA YESU tushindie.

Paulo alipojua hivi, alisema ‘’ Ndugu sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu ; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo , niifikie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa MUNGU katika KRISTO’’ (Wafilipi 3:13-14).

                               TUMEOKOLEWA NA YESU KWELI KWELI.

Mtoto hawezi kukua bila uhai.
uhai unapoaanza  na kukua  kunaanza.
Wanadamu wote wamekufa kiroho kwa ajili ya dhambi. Lakini mtu akitubu na kumwamini YESU KRISTO anapata uzima(uhai). Ndipo kukua kiroho kunaanza.
Wengi wanashuhudia wakisema ‘nimeokoka’. Hawa wanakutana na maswali, ‘unajuaje umeokoka?’. Biblia inasema kwamba tukimwamini BWANA YESU, yaani tukimpokea BWANA YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wetu; tunakuwa na uhusiano naye kibinafsi, basi tumeokoka.(Yohana 1:12).
Siku mtu anapomkaribisha YESU maishani mwake, YESU anaingia na kumfanya mtoto wa MUNGU. Haidhuru anatumia lugha gani kueleza hili, wengine husema ‘Nimeokoka’ au ‘Nampenda YESU’ au ‘Nimeokolewa’ au ‘nimekata shauri kumfuata YESU’ n.k.
Nampenda YESU anayeokoa maana watu hukata shauri kumpokea  YESU   kwa njia tofauti. Wengine wanakuwa kanisani, wengine kwenye mikutano ya injili wengine kwenye semina na wengine nyumbani mwao na wengine huongozwa na rafiki zao kumpokea YESU KRISTO. Na wapo wengine ambao hawakumbuki siku walipompokea YESU wengine wali,pokea kwa njia ya redio. Ila wote hawa ROHO MTAKATIFU alijenga imani ndani yao taratibu wakisoma neno la MUNGU na kushirikiana na wengine. Iwe iwavyo wote wameokoka.

          MAMBO  TUNAYOKUTANA NAYO KWENYE WOKOVU WETU.

1:   Wakati  mwingine hatujisikii kama tumeokoka, hasa baada ya kuona tumejikwaa mara nyingi katika muda fulani. Lakini tujue kuwa kuokoka kwetu hakutegemei jinsi tunavyojisikia. Tunajua tumeokoka kwa sababu tunaamnini Neno la MUNGU na ahadi zake. Biblia inasema ‘’Wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale walioaminio jina lake’’ –Yohana 1:12.  Hii ni kweli , tena ilivyo ni kwamba   jinsi tunavyokua karibu na BWANA mtakatifu ndivyo tunavyozidi kujiona tusivyofaa mbele zake, linalobaki ni kujinyenyekeza zaidi na kumshukuru kwa neema yake na msamaha wa dhambi.

2: Wakati mwingine watu wanatutia mashaka kwa kutudai vitu ambavyo Biblia haivijai. Wanasema ni lazima tunene kwa lugha ndio itajulikana kuwa tumeokoka, au tuwe waumini wa dhehebu fulani tu. Na kama hatukufanya hivyo wanadai hatujaokoka. Biblia inasema tunaokoka kwa kumpa YESU maisha yetu na  na baada yaa hapo tunaukulia wokovu. Kunena kwa lugha ni jambo jema sana maana ROHO MTAKATIFU anakusaidia kuomba na maombi hayo huende moja kwa moja mbinguni bila hata kukusanywa na malaika, ni muhimu sana na kila mwamini ni vizuri kutamani kunena kwa lugha ila wakati mwingine tendo hilo linaweza kutokea baada ya muda kidogo baada ya mtu kuokoka, hivyo anakua ameshaokoka tayari na mengine yanafuata baadae. Kuhusu kanisa la kusali ni muhimu kusali kanisa ambalo kwanza linakubali wokovu, pia linatumia BIBLIA kama msingi wao wao wa mafundisho pia wanakiri Kuokoka. Wanamaombi na pia kanisa ambalo linakemea dhambi hadharani ndilo kanisa sahihi.
MUNGU akubariki sana ndugu, nahakika umejifunza. Pia kama hujampa BWANA YESU maisha yako wakati wa kufanya hivyo ni leo maana hatujui yatakayokuwako kesho, OKOKA ndugu na MUNGU atakubariki sana
         Ni mimi ndugu yako Baraka Audax.
                       Injili ya Kristo Zanzibar.

Comments

  1. Bwana Yesu asifiwe, nibarikiwa sana na somo Ili. Pia nimejisikia furaha kuona school matena class mate analitangaza jina la Yesu kristo

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts