NEEMA MAALUM.



SOMO :   NEEMA  MAALUM.

Neema  maalum.
         Ni  zawadi  ya  kimungu  anayopewa  mwanadamu  asiyestahiri.
         Mfano:Daudi, Essau,Yusufu n,k.
         KAZI  YA  NEEMA  MAALUM.
1:Itanitafta
         Mfano:Daudi  neema  ilipowadia  ya  kuwa  Mfalme  alitafutwa  porini  alipokuwa  akichunga  kondoo,Mbuzi,Ng’ombe  n.k.

Unapofikia  wakati  Mungu  anataka  kukutumia katika  jambo  la  Kimungu  utafuatwa  mahali  popote  utakapokuwa.

Napenda  nikutie   moyo  ndugu  yangu  mpendwa unayesoma  ujumbe  huu  ya  kuwa  Mungu  anao  mpango  mzuri  wa  maisha  yako  na  ndo  maana  leo  umependa  kusoma  ujumbe  huu  wa  Kimungu,wakati  watu  wengine  wanaona  post hii  wanaiacha  wewe  umepata  kuipenda  na  kuisoma.Hiyo  ni  ishara  kubwa  kuwa  Mungu  anakutafta  abadilishe  maisha  yako  na  vizazi  vya  watoto  wako. Naamini  kuwa  utabalikiwa   wewe  na  vizazi vyako  kwa  maana umekubali  kusikia  sauti  ya  Mungu na  kuitii  kwa  kupenda kusoma  ujumbe  wa Mungu.
2: Hubadilisha  jina.
         Mpango  wa  Mungu ukitimia  hata  jina  lako  linabadilika.
Mfano.                                                                                                       Mwanzo  17:5 :   Maneno  ya  Mungu  yanasema :.
Wala jina lako  hutaitwa tena Abramu,kwani  nimekuweka  uwe  Baba  wa  mataifa  mengi.

 na  Isaya  62:2-4. Na  mataifa  wataiona haki  yako,na wafalme  wote watauona  utukufu  wako; nawe utaitwa  jina  jipya,litakalotajwa  kwenye  kinywa  cha Bwana.

Mpendwa  ndugu  yangu  unayesoma  ujumbe  huu ukae  ukijua  kuwa  Mungu  anao mpango  mkubwa wa  amisha   yako  na wewe  na  ndo  maana  hadi  leo  bado  unaendelea  kuishi  na  kulipenda  kulisoma  neno  la  Bwana mahali  popote  unapokuwa  bila  kujali  hali  na  mazingira  uliyopo.

Wakati  wako  ukifika  hata   jina  lako  litabadilika  kama  watu  walizoea  kukuita  majina  mabaya  ya  ovyo  ovyo  sasa  utaitwa  jina  jipya  na  zuri  sana sema  AMEN.

3:  Neema  maalumu  inakulinda  na  dhambi.
-       Kwa  neema  maalum  yusufu  alikataa  kulala  na  mke  wa  POTIFA.
-       Kwa  neema  maalum  Yusufu  alishindwa  kuuwa  na  ndugu  zake.
-       Kwa  neema  maalum  DAUDI alimshinda  GORIATH
-       Kwa  neema  maalum  Yakobo  kauziwa  uzaliwa  wa  kwanza  na  ESSAU.
-       Kwa  neema  maalum  DAUDI alimshinda  GOLIATH.
-       Kwa  neema  maalum  YAKOBO  kauziwa  uzaliwa  wa  kwanza  na  ESSAU.

-       Kwa  neema  maalum  DAUDI alishindwa  kuuawa  na  SAULI                                                                                                                4.  Inakupandisha  cheo                                                                                         1: DAUDI mchungaji  wa  kondoo  na  kuwa     MFALME                                                                                                                                                                                     2:    YUSUFU  kutoka  gerezani  na  kuwa  mkuu  wa  misri.
3:         SAULI  Kutoka  katika  kuchunga  kondoo  na  kuwa  mfalme

Pia tunapata  kuona  kuwa  YUSUFU  cheo  chake  kilipanda  sana katika  ngazi  mbali  mbali:
  1. Kutoka  kuwa  mtumishi  wa  ndani  kuwa  msimamizi  wa wafungwa.
Kutoka  gerezani  na kuwa  waziri  mkuu,msimamizi  wa  chakula  katika  nchi  nzima  ya Misri


Kwa hapo  najua  utakuwa  umebarikiwa  sana  naamini  kwa  imani  kubwa  sana  kuwa  Mungu  wa  mbinguni  atakupandisha  cheon,  nawe  utabarikiwa  wewe  na  uzao  wa  tumbu  lako.

Pokea  kwa imani  kubwa  sana  maana  najua  utapokea  yote  kwa  jina  la  Yesu  aliye  hai.

Ni mimi  ndugu  yako
Baraka  Audax
0717 461006
Injili  ya  Kristo  Zanzibar 
BARIKIWA  SANA.

Comments

Popular Posts